Table Of ContentSOTERIOLOJIA
MAFUNDISHO YA KIKRISTO KUHUSU
WOKOVU
TEOLOJIA PANGILIFU-2
1
Hakimiliki © 2020 Daniel John Seni
Chapa ya January, 2021
Msanifu: Eternal Word and Charity Publishing (EWCP).
Dar es Salaam [+255-755-643-590]
Mchapaji: Truth Printing Press. Dar es Salaam
[+255764425704]
___________________________________
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho
hili inayoweza kuzalishwa tena, au kuboreshwa au
kusambazwa kwa njia yoyote au kwa kubadilisha umbo
au kunakili na kupeleka katika umbo lingine bila idhini
ya mwandishi.
_______________________________________
Maandiko ya Biblia yamechukuliwa kutoka kwenye
Biblia ya Kiswahili Toleo la shule inayotolewa na Swahili
Union Version (SUV).
Tafsiri iliyotumika kwenye marejeleo yaliyokuwa kwenye
lugha ya kiingereza si tafsiri rasmi; hivyo inaweza
kuendelea kuboreshwa kwa kila chapa ya kitabu hiki.
________________________
Msambazaji
Shekinah Mission Centre (SMC)
[email protected]
S.L.P 32807 Dar es Salaam
+255 769 080 629 +255 787 907 347
Madale/Mivumoni, Joshua road, mkabala na Shule ya
Msingi-Atlas/ at Shekinah Presbyterian Church in
Tanzania, Dar es Salaam
TABARUKU
Kwa wanazuoni wote wa teolojia
i
UTANGULIZI
Huu ni mfululizo wa masomo katika uwanja
wa “Teolojia Pangilifu” (Systematic
Theology). Sasa tunashughulikia somo la
Soteriolojia, yaani somo linalohusu “wokovu
wa mwanadamu.”
Siku hizi pengine inaweza kudhaniwa
kwamba kila Mkristo anajua maana ya
wokovu na upatikanaji wake. Watumishi
wengi wasiopenda kujishughulisha huishia
kusema “Yesu anaokoa” bila kufafanua
maana ya sentensi hii nyepesi na rahisi
sana. Ni kweli katika muktadha wa
misiolojia tunaweza kutumia sentensi
nyepesi kama hizi bila kuzitolea ufafanuzi
kwa sababu wale tunaowaambia
tunachukulia kwamba hawajui kitu
chochote.
ii
Siku hizi kuna makanisa yanayojiita,
“makanisa ya wokovu” ambayo hudai
kuhubiri wokovu wa kweli. Hata hivyo,
nimegundua mapungufu mengi katika
mafundisho yao kuhusu wokovu kwa
kudhania kwamba wokovu ni tukio la
sekunde moja.
Ama kwa hakika, wokovu ni mchakato;
ingawa yawezekana michakato hiyo
isipangiliwe vizuri na kuleta maana, lakini
bado tunapaswa kujua kwamba wokovu ni
mchakato. Mchakato wa kumwokoa
mwanadamu unaanzishwa na Mungu
mwenyewe na kumaliziwa pia na Mungu
mwenyewe.
Katika kitabu hiki, kwa namna ya upekee
nimejaribu kufafanua kwa undani kuhusu
michakato hiyo kwa kuzingatia ufafanuzi
iii
wa teolojia iliyoboreshwa (Reformed
Theology)
Kitabu hiki si kwa wale ambao
wameshazaja akili zao mafundisho
mbalimbali ya wokovu, na hivyo hawataki
kubadilisha mwelekeo na kujifunza upya.
Pia kitabu hiki si kwa wazembe, wasiopenda
kushughulisha akili zao. Si kwa wale
wanaopenda kutafuniwa tu, bali ni kwa
wale ambao wanaweza kuvunja mifupa na
kuelewa.
Ninakutia moyo kwamba unaposoma kitabu
hiki unahitaji kusoma katika hali ya
utulivu, na kumwomba Roho Mtakatifu
akusaidie ili uweze kuelewa zaidi na zaidi
somo hili muhimu.
Marejeleo mengi yaliyotumika katika kitabu
hiki yanatokana na lugha ya Kiingereza,
iv
hivyo basi, kwa wale ambao wana uwezo wa
kusoma Lugha ya Kiingereza wanashauriwa
kupata baadhi ya nakala za vitabu hivyo
kwa sababu ni muhimu sana.
Yawezekana katika kitabu hiki ninaweza
nisikubaliane na baadhi ya tafsiri ya kambi
ya Teolojia Iliyoboreshwa kwa asilimia zote,
lakini kwa kweli kwa sehemu kubwa
inakubaliana na mafundisho halisi ya Neno
la Mungu.
v
Yaliyomo
TABARUKU ................................................. i
UTANGULIZI .............................................. ii
Yaliyomo ................................................... vi
SURA YA KWANZA ..................................... 1
Maana ya soteriolojia ............................... 1
Kila Dini Hutafuta Wokovu ...................... 4
Hitaji la Wokovu kwa Mwanadamu .......... 7
Mpango wa Wokovu wa Mungu kwa
Wokovu wa Mwanadamu ....................... 10
Mungu alijua mapema kila kitu ............. 12
Mpango wa Kusudi la Mungu la Milele .. 19
Wito wa Kupokea Wokovu...................... 21
SURA YA PILI ........................................... 25
MPANGILIO WA WOKOVU ........................ 25
SURA YA TATU ......................................... 34
KUCHAGULIWA MAPEMA NA KUITWA ..... 34
vi
a. Kuchaguliwa .................................. 34
Dhana potofu kuhusu kuchaguliwa
mapema ................................................ 42
Majibu kwa dhana potofu ...................... 44
Ni Wateule tu. ........................................ 46
b. Kuitwa ............................................ 55
Maswali fikirishi .................................... 66
SURA YA NNE .......................................... 67
KUZALIWA UPYA NA KUHESABIWA HAKI 68
a. Kuzaliwa Upya................................ 68
b. Kuhesabiwa Haki ........................... 75
SURA YA TANO ........................................ 88
TOBA NA UTAKASO ................................. 88
a. Toba ............................................... 88
b. Utakaso .......................................... 97
SURA YA SITA ........................................ 103
vii